Gossip

Bahati Awachana Watesi Wake Baada ya “Seti” Kufikisha Views Milioni Moja

Bahati Awachana Watesi Wake Baada ya “Seti” Kufikisha Views Milioni Moja

Msanii wa muziki kutoka Kenya, BahatI, ameendelea kusherehekea mafanikio makubwa baada ya wimbo wake wenye utata, “Seti”, kufikisha zaidi views milioni moja ndani ya siku tatu tangu kuzinduliwa kwenye mtandao wa YouTube.

Kupitia mitandao yake ya kijamii, Bahati amedai kuwa amevunja rekodi kwa kuwa msanii wa Kenya mwenye wimbo uliotazamwa zaidi ndani ya saa 24, jambo alilolitaja kuwa ushahidi tosha kwamba bado anatawala muziki wa Kenya.

Bahati hakusita kuwashambulia wakosoaji wake, akisema kuwa licha ya maneno ya chuki na lawama wanazoeneza, mafanikio yake yanaendelea kuongezeka. Ameongeza kuwa wale wanaomkosoa hawana uwezo wa kumzuia, kwani talanta halisi haiwezi kuzimwa na maneno ya mitandaoni.”

Bahati pia amewataka watesi wake kukubali kwamba muziki wake ndio unaongoza kwa sasa, akisisitiza kuwa yuko tayari kuendelea kuvunja rekodi na kuweka viwango vipya katika tasnia ya burudani.

Licha ya maudhui ya wimbo wake “Seti” kuibua mjadala mkali, Bahati amesema ataendelea kufanya muziki unaozungumziwa na kuleta vuguvugu jipya katika sekta ya burudani, akisisitiza kuwa hata chuki ni ushahidi wa mafanikio.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *