Entertainment

Msanii wa Injili Janet Otieno Awabariki Mashabiki na EP Mpya

Msanii wa Injili Janet Otieno Awabariki Mashabiki na EP Mpya

Mwanamuziki wa nyimbo za injili Janet Otieno ameanza msimu mpya wa huduma yake ya muziki kwa kuachia rasmi EP yake ya kwanza iitwayo “Unaposhuka”, ambayo sasa inapatikana katika majukwaa yote ya muziki mtandaoni.

Kupitia ujumbe wake kwa mashabiki, Janet ameeleza kuwa amefurahia sana kuachia kazi hii mpya ambayo imebeba ujumbe wa kumtukuza Mungu.

Msanii huyo amesema EP hiyo imebeba jumla nyimbo sita za moto na ina nyimbo kama Jina Lako, Unaposhuka, Unastahili, Mwamba Imara, Salama na Mwaminifu.

Hata hivyo amesema kuwa hii ni hatua muhimu katika safari yake ya muziki wa injili na ni mwanzo wa msimu mpya wa kuinua mioyo ya mashabiki zake kupitia nyimbo zenye mafunzo na faraja.

Kwa sasa, Unaposhuka EP inapatikana kwenye majukwaa yote ya kusikiliza muziki ikiwemo Spotify, Boomplay, YouTube na Apple Music

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *