
Siku ya jana, YouTube imetangaza katika ukurasa wake wa News & Events, kuwa inaweka mabadiliko mapya ya kuficha jumla ya “Dislikes” katika video. Kwa kawaida, watazamaji wanaweza ku-Like au Dislike video, na idadi ya Likes na Dislikes imekuwa ikionekana chini ya video.
Katika kuzuia ubaguzi, kuwatania Content Creators wadogo na kuzidi kuwapa moyo Content Creators, YouTube imeanza kuweka uwezo wa kuficha idadi ya “Dislikes” katika videos. Bado ukitazama video utaona button ya LIKE na DISLIKE lakini mwenye akaunti tu ndiye ambaye atakuwa na uwezo wa kuona idadi ya Dislikes katika video zake.
Itaanza kuanzia leo na taratibu mabadiliko yataonekana katika video zote. YouTube imesema itakuwa ni lazima na hakuna option kwa content creators kuacha idadi ya dislikes kuonekana; ili kuzuia Content Creator asionekane amezuia idadi ya likes makusudi. Hivyo ni lazima video zote za YouTube zitakuwa hazionyeshi idadi ya Dislikes na mabadiliko haya yameanza taratibu na itakwepo katika video zote za YouTube