Msanii wa Bongo Fleva, Marioo, amefunguka kwa hasira akilalamikia watu maarufu, wanasiasa na marafiki wanaodaiwa kumtongoza mke wake Paula Kajala.
Kupitia instastory, amesema amekuwa akivumilia kwa muda mrefu vitendo vya baadhi ya watu maarufu wanaojaribu kuingilia uhusiano wake, lakini sasa ameamua kuweka mambo hadharani.
Hitmaker huyo wa Dunia, ameeleza kuwa ataweka wazi majina na ushahidi wa mazungumzo ya watu wanaomtongoza mchumba wake, akisisitiza kuwa hana tena uvumilivu.
Msanii huyo pia amefichua kuwa kipindi mpenzi wake alipokuwa na ujauzito, baadhi ya watu walimshawishi kutoa mimba kwa kisingizio kwamba hangemfaa tena, lakini amesema anamshukuru mama mtoto wake kwa kuonyesha ujasiri na msimamo.
Ujumbe huo umechochea maoni mseto mtandaoni, huku mashabiki na wadau wa muziki wakitafsiri maneno ya Marioo kama dalili za msongo wa mawazo au hasira kutokana na mambo ya uhusiano. Wengine wameshauri msanii huyo kutuliza hasira na kushughulikia masuala binafsi nje ya mitandao ya kijamii.