Gossip

Msanii Tipsy Gee Adai Wimbo Mpya wa Toxic Lyrikali Hauna Ubunifu

Msanii Tipsy Gee Adai Wimbo Mpya wa Toxic Lyrikali Hauna Ubunifu

Msanii anayesuasua kisanaa kutoka Kenya, Tipsy Gee, amemtolea uvivu rapa Toxic Lyrikali kwa kuuponda hadharani wimbo mpya wa rapa huyo uitwao “Euphoria.”

Kupitia mitandao ya kijamii, Tipsy Gee ameonekana kutoridhishwa kabisa na ubora wa kazi hiyo, akisema kuwa wimbo huo haukidhi viwango vinavyotarajiwa kutoka kwa msanii ambaye sekta ya muziki inamtegemea.

Tipsy Gee ambaye juzi kati aligeukia muziki wa Mugithi baada ya kushindwa kutamba na Arbatone, amesema kuwa haiwezekani msanii mwenye heshima kama Toxic Lyrikali kutoa wimbo ambao hauna ubunifu wala nguvu ya kushawishi mashabiki.

Ikumbukwe, Tipsy Gee amekuwa mkosoaji mkubwa wa Toxic Lyrikali kwa muda sasa, kitendo ambacho wadau wa muziki nchini Kenya wanahoji kuwa huenda Titoker huyo aliyegeukia muziki anatumia jina la Lyrikali kujitengenezea nafasi katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *