
Staa wa muziki wa hiphop nchini Octopizzo ametangaza kuachia album yake mpya inayokwenda kwa jina la “Motivation”
Octopizzo ameweka wazi hilo kupitia ukurasa wake wa Twitter huku akiwawataka mashabiki zake wakae mkao wa kula kuipokea album hiyo ambayo kwa mujibu wake ipo njiani.
Hitmaker huyo wa “Babylon” amesema mashabiki wanaweza kui-pre-order kupitia majukwaa ya muziki kama Spotify na Apple music ila tayari ameachia ngoma ya kwanza kutoka kwenye album hiyo iitwayo “Motivation”.
Motivation itakuwa ni album ya sita kwa mtu mzima Octopizzo baada ya Jungle Fever iliyotoka mwaka wa 2020 ikiwa na jumla ya mikwaju 15 ya moto.