Entertainment

Wasanii wa Bongo Fleva Watoa Salamu za Pole kwa Familia ya Raila Odinga na Wakenya

Wasanii wa Bongo Fleva Watoa Salamu za Pole kwa Familia ya Raila Odinga na Wakenya

Msiba wa Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya, Raila Amolo Odinga, umeibua wimbi la huzuni na maombolezo kutoka pande mbalimbali za Afrika Mashariki, huku wasanii wakubwa wa Bongo Fleva kutoka Tanzania wakituma salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu na wananchi wa Kenya.

Mastaa wakiongozwa na Ali Kiba, Juma Jux, AY Maua Sama, Joh Makini, H Baba na wengine wengi wameungana kuonyesha masikitiko yao, wakimtaja Raila kama kiongozi wa kipekee, mwenye maono, ujasiri na upendo kwa watu wake.

Kupitia mitandao ya kijamii, wasanii hao wameeleza kuguswa na kifo cha Raila, wakisema kuwa Afrika imepoteza kiongozi aliyeacha alama kubwa katika historia ya siasa na umoja wa bara hili. Wamepongeza maisha yake ya kujitolea kwa haki, demokrasia na usawa, wakisema Raila alikuwa mfano wa kuigwa kwa vizazi vingi vijavyo.

Kwa pamoja, wamewatumia rambirambi kwa Rais William Ruto, familia ya Raila Odinga na wananchi wote wa Kenya, wakisisitiza kuwa wanawaombea faraja, nguvu na utulivu katika kipindi hiki cha maombolezo.

Mashabiki kutoka pande zote za Afrika Mashariki wamepongeza hatua hiyo ya wasanii wa Tanzania, wakisema ni ishara ya umoja wa kijamii na kiutamaduni uliopo kati ya Kenya na Tanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *