Entertainment

Otile Brown Aandaa Wimbo Maalum Kumheshimu Hayati Raila Odinga

Otile Brown Aandaa Wimbo Maalum Kumheshimu Hayati Raila Odinga

Mwanamuziki nyota wa Kenya, Otile Brown, ametangaza kuwa yuko mbioni kukamilisha wimbo maalum wa kumuenzi aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya, hayati Raila Amolo Odinga.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Otile ameshiriki kipande cha video akiwa studioni akirekodi mradi huo wa kihisia, akieleza kuwa alihitaji muda wa kuhakikisha kazi hiyo inatoka kwa moyo wake kabisa.

Msanii huyo amesema kuwa hayati Raila alikuwa mtu wa heshima kubwa na anastahili kutambuliwa kwa mchango wake mkubwa kwa taifa la Kenya. Otile ameahidi kutoa wimbo huo hivi karibuni kama njia ya kutoa heshima na upendo wake kwa kiongozi huyo aliyegusa maisha ya wengi.

Taarifa hii inakuja siku ambayo Raila Odinga amepumzishwa kwenye nyumba yake ya milele huko Bondo, Kaunti ya Siaya, katika mazishi yaliyohudhuriwa na viongozi wa kitaifa, wageni wa kimataifa na maelfu ya waombolezaji waliokusanyika kumuenzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *