LifeStyle

Bahati Aadhimisha Miaka 9 ya Ndoa, Aahidi Zawadi Tisa kwa Mkewe

Bahati Aadhimisha Miaka 9 ya Ndoa, Aahidi Zawadi Tisa kwa Mkewe

Msanii wa muziki nchini Kenya, Bahati, anaadhimisha miaka 9 ya ndoa yake na mkewe Diana Marua, akifichua kuwa anapanga kutoa zawadi tisa kuashiria kila mwaka wa mapenzi yao.

Kupitia mitandao ya kijamii, Bahati ameeleza furaha yake kwa kufikisha miaka tisa katika ndoa, akisema kuwa safari yao imekuwa ya baraka na mafanikio.

Msanii huyo, ameomba mashabiki wake kupendekeza aina ya zawadi anayopaswa kumpa mke wake mwaka huu, akisisitiza kuwa zawadi zote tisa tayari ameziandaa kwa ajili ya mke wake huyo.

Bahati amekuwa na utamaduni wa kutoa zawadi kila mwaka kulingana na muda wao wa kudumu kwenye ndoa, jambo ambalo limekuwa likiwavutia mashabiki wake wengi mtandaoni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *