Rais wa shirikisho la wanamuziki nchini Uganda, Eddy Kenzo, amefunguka kuhusu ukosoaji unaoendelea baada ya baadhi ya watu kudai kuwa Kenzo na wasanii wenzake walinufaika kifedha kupitia ushiriki wao katika albamu ya muziki ya kusifu uongozi wa Rais Yoweri Museveni,
Akizungumza Tiktok Live, Kenzo amesema hakuna msanii aliyelipwa kushiriki kwenye albamu hiyo, akieleza kuwa walifanya kazi hiyo kwa hiari kama zawadi kwa Rais Museveni wakimshukuru kutokana na mchango wake katika sekta ya muziki na taifa kwa jumla.
Msanii huyo, amefafanua kuwa yeye na wasanii wenzake walishiriki katika mradi huo kwa nia ya kuonyesha shukrani kwa amani na uhuru ambao Rais amesaidia kuleta katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
Kwa sasa, albamu hiyo inaendelea kujadiliwa kwenye mitandao ya kijamii, baadhi ya wananchi wakiiona kama ishara ya uzalendo, huku wengine wakiiita propaganda ya kisiasa