Sports news

Arsenal Yadhibu Atlético Madrid Mabao 4-0 Uwanjani Emirates

Arsenal Yadhibu Atlético Madrid Mabao 4-0 Uwanjani Emirates

Klabu ya Arsenal imeanza kampeni zao za Ligi ya Mabingwa kwa kishindo baada ya kuichapa Atlético Madrid kwa mabao 4–0 katika mchezo uliopigwa usiku wa Jumanne kwenye uwanja wa Emirates, London.

Timu hiyo ya kocha Mikel Arteta ilionyesha kiwango cha kuvutia katika kipindi cha pili, baada ya kipindi cha kwanza kumalizika bila timu yoyote kupata goli. Katika kipindi cha pili cha mchezo, Arsenal ilionyesha ubora wake kwa kufunga mabao manne ndani ya dakika 13.

Gabriel Magalhãesalifungua ukurasa wa mabao kwa kichwa cha nguvu akimalizia mpira wa mkwaju wa bure kutoka kwa Declan Rice katika dakika ya 57. Dakika 7 baadaye, Gabriel Martinelli aliongeza bao la pili kwa shuti kali lililomshinda kipa Jan Oblak. Viktor Gyökeres alifunga mabao mawili kwa mfululizo katika dakika ya 67 na 70, akimaliza ukame wa mabao wa mechi tisa.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, amekiri kuwa timu yake ilicheza kwa umoja na ari, akisisitiza umuhimu wa kuendelea na kasi hii katika mechi zijazo. Kwa upande mwingine, kocha wa Atlético Madrid, Diego Simeone, alikiri makosa ya kiufundi yaliyosababisha kipigo hicho.

Kwa ushindi huu, Arsenal inaendelea kuwa na rekodi safi ya ushindi katika makundi ya Champions League, ikiwa na pointi 9 na mabao 4 bila kuruhusu nyavu zao kuguswa. Atlético Madrid, licha ya kuanza vizuri, sasa ina pointi 3 baada ya mechi tatu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *