VAR na Raya Waibeba Arsenal London Stadium; Yaichapa West Ham 1-0

VAR na Raya Waibeba Arsenal London Stadium; Yaichapa West Ham 1-0

Arsenal imevuka kigingi kigumu katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) baada ya kuibuka na ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya West Ham United katika dimba la London Stadium. Katika mtanange uliotawaliwa na upinzani mkali, Leandro Trossard aliibuka shujaa wa ‘Washika Bunduki’ kwa kupachika bao la ushindi dakika ya 83 akimalizia pasi safi ya nahodha Martin Ødegaard. Hata hivyo, ushindi huo haukuja kirahisi, kwani ulihitaji uingiliaji wa teknolojia na uhodari wa kipa kulinda alama tatu. Mchezo ulifikia kilele cha msisimko pale West Ham walipofunga bao la kusawazisha kupitia kwa Callum Wilson katika dakika za nyongeza. Hata hivyo, mwamuzi alilipeleka tukio hilo kwenye VAR, ambapo ilionekana kuwa kipa wa Arsenal, David Raya,alichezewa rafu kabla ya mpira kuingia wavuni. Mbali na msaada wa VAR, David Raya alikuwa nyota wa mchezo baada ya kuokoa michomo kadhaa ya hatari (saves), ikiwemo shuti la karibu la Mateus Fernandes, na hivyo kuwahakikishia Arsenal ushindi huo muhimu ugenini. Matokeo haya yanaiweka Arsenal kileleni mwa msimamo ikiwa na alama tano mbele ya wapinzani wao wakuu, Manchester City, ingawa City wana mchezo mmoja mkononi. Arsenal sasa inahitaji kushinda mechi zake mbili zilizosalia dhidi ya Burnley na Crystal Palace ili kutangazwa mabingwa wapya. Kwa West Ham, kichapo hiki kinawaacha katika wakati mgumu wakipambana kutoshuka daraja, huku mashabiki wao wakiondoka London Stadium wakiwa na malalamiko dhidi ya maamuzi ya VAR.

Read More
 Arsenal Yatinga Robo Fainali ya FA Cup kwa Ushindi Dhidi ya Mansfield Town

Arsenal Yatinga Robo Fainali ya FA Cup kwa Ushindi Dhidi ya Mansfield Town

Arsenal imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya Kombe la FA (FA Cup) baada ya kupata ushindi wa tabu wa mabao 2-1 dhidi ya Mansfield Town katika mchezo uliopigwa leo, Machi 7, 2026, kwenye uwanja wa One Call Stadium Arsenal walitangulia kwa bao safi la Noni Madueke dakika 41 baada ya kazi nzuri ya pamoja, bao lililodumu hadi mapumziko. Mansfield Town walirejea kwa kasi kipindi cha pili ambapo mchezaji wa akiba, Will Evans, alileta mshangao uwanjani kwa kufunga bao la kusawazisha dakika 50 na kufanya matokeo kuwa 1-1. Baada ya hali kuwa ngumu, Arteta alimuingiza Eberechi Eze ambaye alihitaji dakika chache tu kupachika bao la ushindi dakika ya 66 na kuzima ndoto za Mansfield. Ushindi huo ni wa tano mfululizo kwa Arsenal katika mashindano yote, ukiendeleza kasi yao nzuri ya msimu huu ambapo pia wanaongoza msimamo wa Ligi Kuu (EPL) kwa pointi 67. The Gunners sasa wanageuza macho yao kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League). Watasafiri kuvaana na Bayer Leverkusen nchini Ujerumani kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya 16 bora, utakaopigwa Jumatano, Machi 11, 2026.

Read More
 Arsenal Yaendelea Kuchanja Mbuga Kileleni mwa EPL

Arsenal Yaendelea Kuchanja Mbuga Kileleni mwa EPL

Klabu ya Arsenal imeendeleza kasi yake ya kusaka taji la Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu baada ya kuibuka na ushindi muhimu wa 1-0 dhidi ya Brighton & HoveAlbion katika uwanja wa Amex. Bao la pekee la mshambuliaji Bukayo Saka katika dakika ya 9 lilitosha kuwapa Gunners alama tatu muhimu na kuongeza mwanya wa uongozi kileleni kufikia alama saba. Wakati Arsenal ikisherehekea, mahasimu wao Manchester City walipoteza alama muhimu nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 na Nottingham Forest. City walitangulia kwa mabao ya Antoine Semenyo na  Rodri lakini Forest walipambana na kusawazisha kupitia Morgan Gibbs-White na Elliot Anderson, matokeo yaliyowaacha mabingwa hao watetezi wakiwa nyuma kwa alama saba dhidi ya Arsenal. Katika mechi nyingine zilizopigwa jana usiku, Chelsea walipata ushindi mnono wa 4-1 ugenini dhidi ya Aston Villa, huku João Pedro aking’ara kwa kufunga hat-trick.Newcastle United waliibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Manchester United katika dimba la St. James’ Park. West Ham United waliondoka na ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Fulham ugenini.

Read More
 Arsenal Yatinga Fainali ya Carabao Cup Baada ya Ushindi Dhidi ya Chelsea

Arsenal Yatinga Fainali ya Carabao Cup Baada ya Ushindi Dhidi ya Chelsea

Klabu ya Arsenal imefuzu kwa fainali ya Carabao Cup baada ya kuibwaga Chelsea kwa bao 1–0 katika mchezo wa marudiano uliopigwa kwenye Uwanja wa Emirates. Bao pekee la mchezo huo lilifungwa na Kai Havertz katika dakika ya 96, akimalizia ushindi wa jumla wa mabao 4–2 kwa Gunners katika hatua ya nusu fainali ya mikondo miwili. Havertz, ambaye aliwahi kuichezea Chelsea, alihakikisha Arsenal inasonga mbele kwa kuipa timu yake goli la ushindi wa dakika za mwisho. Kwa matokeo haya, Arsenal sasa itasubiri mshindi kati ya Manchester City na Newcastle United ili kukutana naye katika fainali itakayochezwa Wembley mnamo Machi 22, 2026. Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, alisifu nidhamu na ari ya wachezaji wake, akisema kuwa kufuzu kwa fainali ni ushahidi wa maendeleo ya timu msimu huu

Read More
 Arsenal Yakubali Kichapo cha Nyumbani Emirates Dhidi ya Man United

Arsenal Yakubali Kichapo cha Nyumbani Emirates Dhidi ya Man United

Klabu ya Arsenal imekubali kichapo cha mabao 3-2 kutoka kwa Manchester United katika mchezo uliopigwa leo katika dimba la Emirates Stadium. Arsenal walianza kwa furaha baada ya beki wa United, Lisandro Martinez, kujifunga bao dakika ya 29 na kuwapa wenyeji uongozi wa muda. Hata hivyo, United walirejea mchezoni dakika ya 37 kupitia kwa Bryan Mbeumo aliyesawazisha bao hilo kabla ya mapumziko. Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Patrick Dorgu akiipatia Manchester United bao la pili dakika ya 50, na kuifanya Arsenal kuanza msako wa kusawazisha. Juhudi zao zilifanikiwa dakika ya 84 kupitia kwa Mikel Merino aliyefunga bao la pili kwa upande wa Arsenal. Lakini furaha ya Arsenal haikudumu kwa muda baada ya Matheus Cunha kufunga United bao la ushindi dakika ya 87, na kuwamaliza kabisa matumaini ya wenyeji kupata pointi nyumbani. Licha ya kipigo, Arsenal wanasalia kileleni mwa Ligi Kuu England na pointi 50, huku United wakipanda hadi nafasi ya nne wakiwa na pointi 38.

Read More
 Arsenal Watinga Raundi ya Nne Baada ya Kulaza Portsmouth 4-1

Arsenal Watinga Raundi ya Nne Baada ya Kulaza Portsmouth 4-1

Washika Mitutu, Arsenal, wamepiga hatua kubwa katika Kombe la FA baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Portsmouth katika mchezo wa raundi ya tano. Mashabiki wa Portsmouth walipata furaha ya mapema baada ya Bishop kufunga bao dakika ya 3 na kuipa timu yake uongozi. Hata hivyo, matumaini hayo yalidumu kwa muda mfupi tu, kwani Dozzell alijifunga dakika ya 8 na kuisawazishia Arsenal. Dakika ya 25, Martinelli alionyesha makali yake kwa kufunga bao la pili na kuipa Arsenal uongozi. Baada ya mapumziko, kijana huyo aliongeza bao la tatu dakika ya 51, kabla ya kukamilisha ‘hat-trick’ yake dakika ya 72 na kuhitimisha ushindi wa kishindo kwa Washika Mitutu. Matokeo haya yanawaweka Arsenal katika nafasi nzuri ya kuendeleza safari yao ya kutafuta taji la Kombe la FA huku mashabiki wakibaki na matumaini makubwa ya kutwaa kombe

Read More
 Arsenal Yadhibu Atlético Madrid Mabao 4-0 Uwanjani Emirates

Arsenal Yadhibu Atlético Madrid Mabao 4-0 Uwanjani Emirates

Klabu ya Arsenal imeanza kampeni zao za Ligi ya Mabingwa kwa kishindo baada ya kuichapa Atlético Madrid kwa mabao 4–0 katika mchezo uliopigwa usiku wa Jumanne kwenye uwanja wa Emirates, London. Timu hiyo ya kocha Mikel Arteta ilionyesha kiwango cha kuvutia katika kipindi cha pili, baada ya kipindi cha kwanza kumalizika bila timu yoyote kupata goli. Katika kipindi cha pili cha mchezo, Arsenal ilionyesha ubora wake kwa kufunga mabao manne ndani ya dakika 13. Gabriel Magalhãesalifungua ukurasa wa mabao kwa kichwa cha nguvu akimalizia mpira wa mkwaju wa bure kutoka kwa Declan Rice katika dakika ya 57. Dakika 7 baadaye, Gabriel Martinelli aliongeza bao la pili kwa shuti kali lililomshinda kipa Jan Oblak. Viktor Gyökeres alifunga mabao mawili kwa mfululizo katika dakika ya 67 na 70, akimaliza ukame wa mabao wa mechi tisa. Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, amekiri kuwa timu yake ilicheza kwa umoja na ari, akisisitiza umuhimu wa kuendelea na kasi hii katika mechi zijazo. Kwa upande mwingine, kocha wa Atlético Madrid, Diego Simeone, alikiri makosa ya kiufundi yaliyosababisha kipigo hicho. Kwa ushindi huu, Arsenal inaendelea kuwa na rekodi safi ya ushindi katika makundi ya Champions League, ikiwa na pointi 9 na mabao 4 bila kuruhusu nyavu zao kuguswa. Atlético Madrid, licha ya kuanza vizuri, sasa ina pointi 3 baada ya mechi tatu.

Read More
 Arsenal Yaomboleza Kifo Cha Raila Odinga

Arsenal Yaomboleza Kifo Cha Raila Odinga

Klabu ya Arsenal imejiunga na mamilioni ya waombolezaji duniani kote kuomboleza kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Amolo Odinga, ikimtaja kama kiongozi mwenye maono, aliyependa maendeleo na kuhimiza amani. Kupitia taarifa rasmi, miamba hao wa soka wa Uingereza wametuma salamu za rambirambi kwa taifa la Kenya na familia ya Odinga, wakisema Raila alikuwa mtu mwenye ushawishi mkubwa na shabiki wa dhati wa timu hiyo. Raila alikuwa mashabiki maarufu wa Arsenal, akifuatilia kwa karibu michezo yao na kuhudhuria mechi kadhaa katika uwanja wa Emirates jijini London. Mara yake ya mwisho kushuhudia pambano la Arsenal ilikuwa mwezi Machi mwaka 2022, wakati kikosi hicho kilipomenyana na Liverpool. Kifo cha Raila Odinga kimezua majonzi makubwa si tu nchini Kenya bali pia duniani kote, huku viongozi, mashirika na mashabiki wa michezo wakitoa salamu za pole kwa familia yake na wananchi wa Kenya

Read More
 Arsenal Yaibuka na Ushindi Mnono Dhidi ya Manchester United Ugenini

Arsenal Yaibuka na Ushindi Mnono Dhidi ya Manchester United Ugenini

Klabu ya Arsenal imeanza msimu mpya kwa kishindo baada ya kuibuka na ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Manchester United katika uwanja wa Old Trafford, katika mechi ya kwanza ya msimu wa ligi kuu ya Uingereza. Bao pekee la mchezo huo lilifungwa mapema dakika ya 13 na beki mpya wa Arsenal, Riccardo Calafiori, aliyemalizia kona kwa ustadi na kuzamisha matumaini ya mashabiki wa nyumbani. Goli hilo lilitosha kuipa Arsenal alama zote tatu dhidi ya wapinzani wao wa jadi. Kwa ushindi huu, Arsenal inaendelea kuonyesha ubabe wake dhidi ya Mashetani Wekundu, ikiwa ni ushindi wao wa tano katika mechi sita za mwisho dhidi ya Manchester United. Aidha, The Gunners hawajapoteza mchezo katika dimba la Old Trafford kwa zaidi ya miaka mitatu, rekodi inayowapa morali kubwa katika mbio za ubingwa msimu huu. Manchester United, kwa upande wao, watalazimika kujitathmini mapema baada ya kuanza msimu kwa kipigo nyumbani. Mashabiki wao walionekana kukata tamaa mapema kutokana na ukosefu wa ubunifu katika safu ya ushambuliaji na mapungufu katika safu ya ulinzi.

Read More
 Kieran Tierney Arejea Celtic kwa Mkataba wa Miaka Mitano

Kieran Tierney Arejea Celtic kwa Mkataba wa Miaka Mitano

Klabu ya Celtic imethibitisha kumsajili beki wa kushoto Kieran Tierney kwa mkataba wa miaka mitano, akisajiliwa kama mchezaji huru baada ya kuachana rasmi na Arsenal. Tierney, mwenye umri wa miaka 28, anarudi nyumbani katika klabu alikolelewa kisoka, baada ya miaka sita ya kuichezea Arsenal tangu alipojiunga nao mwaka 2019 kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 25. Katika kipindi chake na The Gunners, raia huyo wa Scotland alicheza jumla ya mechi 144 na kufunga mabao sita, akitoa mchango mkubwa hasa katika mafanikio ya awali ya kocha Mikel Arteta, ikiwa ni pamoja na kushinda Kombe la FA mwaka 2020. Usajili wa Tierney unachukuliwa kama hatua muhimu kwa Celtic, wakijaribu kuimarisha kikosi chao kwa msimu ujao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya Scotland. Mashabiki wa Celtic wamepokea taarifa hiyo kwa shangwe, wakimkaribisha mchezaji ambaye si tu ni kipenzi chao bali pia ni zao la akademia ya klabu hiyo, na aliwahi kuwa nahodha chipukizi kabla ya kuondoka kuelekea Ligi Kuu ya England. Kwa sasa, mashabiki wanatazamia kuona iwapo kurejea kwa Tierney kutazidi kuimarisha safu ya ulinzi ya Celtic na kuwapa ushindani mkubwa ndani na nje ya nchi.

Read More
 Arsenal Yatoa Ofa ya Pauni 59 Milioni kwa Viktor Gyokeres wa Sporting

Arsenal Yatoa Ofa ya Pauni 59 Milioni kwa Viktor Gyokeres wa Sporting

Klabu ya Arsenal imeanza mazungumzo rasmi na wakala wa mshambuliaji wa Sporting Lisbon, Viktor Gyokeres, jijini Lisbon, Ureno. Lengo la mazungumzo hayo ni kuhakikisha wanamnasa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Sweden, ambapo tayari Arsenal imewasilisha ofa ya Pauni milioni 59. Ingawa mazungumzo bado yanaendelea, Sporting imeonyesha utayari wa kumwachia Gyokeres kwa kiasi hicho, kutokana na heshima aliyoionyesha klabu hiyo kwa kukataa kuondoka katika dirisha la usajili la majira ya baridi, licha ya kupokea ofa kubwa kutoka klabu mbalimbali. Gyokeres, ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2028, amekuwa na msimu wa kuvutia akiwa na Sporting, akifunga mabao 54 na kutoa asisti 13 katika mechi 52 za michuano yote. Arsenal inamtazama kama chaguo bora kuimarisha safu yake ya ushambuliaji kwa msimu ujao.

Read More
 Arsenal Yaizamisha Newcastle, Yajihakikishia Nafasi ya Pili na Tiketi ya Ligi ya Mabingwa

Arsenal Yaizamisha Newcastle, Yajihakikishia Nafasi ya Pili na Tiketi ya Ligi ya Mabingwa

Arsenal waliendeleza ubabe wao nyumbani kwa kuilaza Newcastle United kwa bao 1-0 katika mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza iliyopigwa Jumapili, Mei 18, 2025, kwenye dimba la Emirates. Ushindi huo umeiwezesha The Gunners kufikisha pointi 71 na kuthibitisha nafasi yao ya pili kwenye msimamo wa ligi, nyuma ya mabingwa wa msimu huu, Liverpool. Katika mechi hiyo, Arsenal walitawala kwa muda mrefu na kuilazimisha Newcastle kucheza kwa tahadhari kubwa, huku wageni hao wakishindwa kutengeneza nafasi za wazi za kufunga. Bao pekee la mchezo lilipatikana dakika ya 55 kupitia kiungo Declan Rice, aliyefunga kwa kichwa baada ya kona ya Bukayo Saka. Newcastle, ambao wapo katika harakati za kuwania nafasi ya kufuzu kwa michuano ya Ulaya, walionekana kuandamwa na presha nzito kutoka kwa Arsenal katika vipindi vyote vya mchezo. Mashambulizi ya Arsenal yalikuwa ya kasi, huku safu ya kati na ya mbele ikidhibiti mchezo kwa ustadi. Kwa matokeo hayo, Newcastle wanasalia na alama 66, sawa na Chelsea na Aston Villa, na sasa wanategemea matokeo ya mwisho ya msimu ili kufuzu kwa mashindano ya bara Ulaya. Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, aliwapongeza vijana wake kwa ushindi huo muhimu na kusema kuwa kurejea kwao katika Ligi ya Mabingwa ni ushahidi wa maendeleo ya klabu msimu huu. Mashabiki wa Arsenal walijitokeza kwa wingi na kusherehekea ushindi huo, wakitazamia kurejea kwa klabu yao katika jukwaa la kifahari barani Ulaya msimu ujao. Mashabiki wa soka sasa wanasubiri kwa hamu mechi ya mwisho ya msimu itakayoweka mambo bayana kuhusu nafasi za Ulaya.

Read More