LifeStyle

Daddy Owen Atoa Kauli Kali Dhidi ya Wanaodhihaki Watu Wenye Ulemavu

Daddy Owen Atoa Kauli Kali Dhidi ya Wanaodhihaki Watu Wenye Ulemavu

Msanii na mwanaharakati wa watu wenye ulemavu, Daddy Owen, ameonyesha masikitiko makubwa kufuatia tabia ya baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii kutumia majukwaa yao kuwakejeli na kuwadharau watu wenye ulemavu.

Kupitia ujumbe wake, Daddy Owen amesema amesikitishwa sana na watu wanaotumia mitandao vibaya kwa kudhalilisha wengine kutokana na hali zao za ulemavu, akisema vitendo hivyo ni vya aibu na havina nafasi katika jamii yenye utu na heshima.

Ameonya kuwa matendo kama hayo yanachochea utekelezaji mkali wa sheria kama vile Cybercrime Bill, akisema jamii isiwe chanzo cha serikali kutumia makosa ya wachache kama kisingizio cha kudhibiti uhuru wa maoni na haki za msingi za binadamu.

Daddy Owen amekumbusha umma kuwa ulemavu si jambo la ajabu bali ni hali ambayo mtu yeyote anaweza kuipata wakati wowote wa maisha, aidha kwa kuzaliwa nayo au kutokana na ajali na magonjwa.

Hata hivyo amemalizia kwa kunukuu methali ya Kiswahili akisema, “Usitukane wakunga na uzazi ungalipo,” akisisitiza umuhimu wa huruma, heshima na utu kwa watu wote bila ubaguzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *