LifeStyle

Akothee Akosoa Vikali Wanaodhihaki Maumbile ya Raila Odinga Junior

Akothee Akosoa Vikali Wanaodhihaki Maumbile ya Raila Odinga Junior

Msanii kutoka Kenya, Akothee, ameonyesha masikitiko makubwa kufuatia dhihaka zinazomlenga Raila Odinga Junior, mwana wa hayati Raila Amolo Odinga, baada ya picha na video kusambaa mitandaoni zikionyesha baadhi ya watu wakicheka maumbile yake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Akothee amelaani vikali tabia ya baadhi ya watu kutumia mitandao vibaya kwa kumkejeli Junior kutokana na maumbile yake. Amesema kizazi cha sasa kimepoteza utu, heshima na huruma, na kwamba baadhi ya vijana wanatumia mitandao ya kijamii vibaya kutokana na malezi duni.

Msanii huyo amesema kuwa matendo kama hayo yakiachwa bila kudhibitiwa yanaweza kuchochea unyanyasaji hata kwa watu wenye ulemavu mitaani. Amesisitiza kuwa vijana wanaohusika lazima wachukuliwe hatua za kisheria ili wajifunze kuishi kwa heshima na utu katika jamii.

Aidha, Akothee amemtumia ujumbe wa faraja Raila Junior, akimtaja kama shujaa anayestahili upendo na heshima kutoka kwa Wakenya. Pia amempongeza Mama Ida Odinga kwa uvumilivu wake na kuahidi kupigania heshima ya familia hiyo, akisema yuko tayari kushughulikia suala hilo kwa ukaribu.

Kauli ya Akothee imezua mjadala mkubwa mitandaoni, wengi wakimpongeza kwa kusimama kidete dhidi ya unyanyasaji wa mtandaoni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *