Mjasiriamali na socialite Zari Hassan amefichua kuwa kisanduku chake cha ujumbe mtandaoni kimefurika na jumbe kutoka kwa wanaume wanaomfuata kwa nia ya kimapenzi.
Kupitia mitandao yake ya kijamii, mama huyo wa watoto watano ameonyesha kuchoshwa na wingi wa wanaume wanaomwandikia kwa sababu zisizo sahihi, akisema wengi wao hawana nia ya dhati bali wanatafuta njia ya kumpotezea muda.
Zari, ambaye kwa sasa ameolewa na bondia na mbunifu wa mitindo kutoka Uganda Shakib Cham, amebainisha kuwa idadi kubwa ya wanaume hao wanamtafuta kwa tamaa na si kwa uhusiano wa maana.
Socialite huyo anayejulikana kwa jina la The Boss Lady amewahi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na msanii wa muziki kutoka Tanzania Diamond Platnumz pamoja na marehemu mfanyabiashara Ivan Semwanga, ambaye wana watoto pamoja.