 
									Mwanamuziki wa injili kutoka nchini Kenya, Justina Syokau, ameonyesha ishara ya heshima na upendo kwa hayati Raila Odinga kwa kunyoa nywele zake zote.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Syokau aMEposti video akiwa saloon akinyolewa nywele na kueleza kuwa aliamua kufanya hivyo ili kumheshimu na kumuomboleza Baba Raila Odinga.
Lakini pia amebainisha kuwa amerekodi wimbo maalum wa kumbukumbu kama sehemu ya heshima yake kwa kiongozi huyo mashuhuri.
Hata hivyo Syokau amesema kitendo hicho ni njia yake ya kuonyesha upendo na kuthamini mchango mkubwa wa kisiasa na kijamii alioutoa Raila kwa taifa la Kenya.
 
								 
             
             
                             
                             
                             
                             
                             
                             
                            