Gossip

Ringtone Apatwa na Kizaazaa Baada ya Tiktoker Kuvuruga Huduma ya Mahubiri Mtandaoni

Ringtone Apatwa na Kizaazaa Baada ya Tiktoker Kuvuruga Huduma ya Mahubiri Mtandaoni

Msanii wa nyimbo za injili, Ringtone Apoko, amejipata katika hali ya sintofahamu baada ya tukio lisilo la kawaida kutokea wakati wa huduma yake ya mahubiri kupitia TikTok Live.

Kwa mujibu wa video iliyosambaa mtandaoni, msanii huyo alikuwa akihubiri na kuwasihi wafuasi wake kumrudia Mwenyezi Mungu, wakati ghafla Tiktoker mmoja mrembo aliingilia kati matangazo hayo ya moja kwa moja na kuanza kumtuhumu Ringtone kwa kupotosha umma.

Hata hivyo, hali ilibadilika zaidi wakati mrembo huyo alianza kumtaka kimahaba msanii huyo, akitumia lugha ya matusi na maneno yasiyokuwa na staha, jambo lililowashangaza watazamaji wa kipindi hicho.

Ringtone, ambaye alionekana akijaribu kumtuliza mrembo huyo kwa busara, alilazimika kusitisha huduma hiyo ya moja kwa moja kutokana na mazungumzo hayo ya aibu ambayo yalikuwa yakimvunjia heshima mbele ya mashabiki wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *