Entertainment

Nandy Afunguka Sababu za Kutumia AI Kwenye Video ya Sweety

Nandy Afunguka Sababu za Kutumia AI Kwenye Video ya Sweety

Msanii nyota wa Bongo Fleva, Nandy, amefunguka sababu kuu ya kutumia teknolojia ya Artificial Intelligence (AI) katika utayarishaji wa video ya wimbo wake uitwao Sweety aliomshirikisha Jux, akisema hatua hiyo ilikuwa ya kulinda ndoa na heshima za kifamilia.

Kwenye mahojiano hivi karibuni, Nandy amesema wazo la kutumia AI lilitokana na tahadhari baada ya kutambua kuwa baadhi ya mashabiki wanaweza kutafsiri vibaya maudhui ya video hiyo endapo wangeonekana pamoja katika baadhi ya sehemu zenye hisia za kimahaba.

Amesema kama msanii aliyeolewa, anapaswa kuwa makini na aina ya kazi anazofanya ili kuepuka kuzua tafsiri zisizofaa kwa mume wake na mashabiki wake.

Aidha, Nandy ameeleza kuwa teknolojia ya AI imesaidia kufanikisha video yenye ubora wa kimataifa bila wao kuhitaji kuigiza kwa pamoja.

Hatua hiyo pia imeonyesha namna muziki wa Afrika Mashariki unavyoweza kutumia ubunifu wa kisasa kutatua changamoto za kijamii bila kuathiri ubora wa kazi za sanaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *