 
									Socialite mwenye asili ya Uganda, Zari Hassan, ametoa onyo kali kwa wanawake kuhusu kupata watoto bila maandalizi ya kifedha.
Zari anasema katika dunia ya sasa, upendo pekee hauwezi kuendesha familia, akisisitiza kwamba wanawake wanapaswa kuwa na uhuru wa kifedha ili kuishi na kulea watoto bila kutegemea wanaume.
Mwanamama huyo wa watoto watano, ameeleza kuwa ni muhimu kwa mwanamke kujijengea msingi imara wa kiuchumi kabla ya kuingia kwenye majukumu ya uzazi, kwani mahusiano yanaweza kubadilika ghafla.
Kwa mujibu wa Zari, mahusiano yanayojengwa tu kwa mapenzi au mvuto wa kimwili mara nyingi hayadumu, na mwisho wa siku wanawake wengi huishia kulea watoto wao pekee.
Hata hivyo amesema kuwa mwanamke ambaye hana uwezo wa kifedha hana sababu ya kupata mtoto hadi atakapokuwa imara kiuchumi.
 
								 
             
             
                             
                             
                             
                             
                             
                             
                            