Gossip

Mashabiki Wazua Gumzo Kuhusu Ujauzito wa Mke wa Stevo Simple Boy

Mashabiki Wazua Gumzo Kuhusu Ujauzito wa Mke wa Stevo Simple Boy

Wajuzi wa mambo na mashabiki mtandaoni wameibua gumzo kubwa wakitilia shaka ujauzito wa mke wa msanii Stevo Simple Boy, wakidai kuwa ameonekana kuwa mjamzito kwa muda mrefu zaidi ya kawaida.

Kwenye mijadala mitandaoni, baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wamedai kuwa ujauzito huo huenda unatumika kama kiki ya kumtangaza Stevo kwenye mitandao badala ya hali halisi ya uzazi. Wengine wameenda mbali zaidi wakitaka uongozi wa msanii huyo kumtafutia Stevo mke halisi, wakihisi kuwa anatumika vibaya kwa masuala ya kujitafutia umaarufu.

Baadhi ya mashabiki wamesema kuwa hali hiyo inamkosea heshima Stevo Simple Boy, ambaye mara kwa mara amekuwa akijulikana kwa unyenyekevu na maisha ya kawaida. Wamesema kuwa msanii huyo anapaswa kulindwa dhidi ya watu wanaotumia jina lake kwa maslahi binafsi.

Licha ya tetesi hizo kusambaa, Stevo Simple Boy na mkewe hawajatoa kauli rasmi kuhusu madai hayo, huku mashabiki wakingoja ufafanuzi zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *