Gossip

Willy Paul Awakosoa Wasanii Anaodai Kula Pesa za Wamama

Willy Paul Awakosoa Wasanii Anaodai Kula Pesa za Wamama

Msanii nyota wa muziki nchini Kenya, Willy Paul, ametoa kauli tata akijisifia kuwa yeye pekee ndiye msanii ambaye hajawahi kula pesa za wamama, huku akiwakosoa wasanii wenzake kwa kutumia wanawake kama chanzo cha kipato na kiki.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Willy Paul amejipongeza kwa kusema kuwa yeye ndiye msanii pekee ambaye hajawahi kuishi kwa kutegemea wanawake, akiwashauri wasanii wenzake kuacha tabia hiyo na kujitafutia mafanikio kwa kazi zao. Ameongeza kuwa kuna baadhi ya wasanii waliokuwa wakitegemea wanawake matajiri lakini kwa sasa wameachwa na wako kwenye msongo wa mawazo.

Katika ujumbe huo huo, Willy Paul amewageukia wasanii wanaovaa mavazi ya kike, akionekana kumtupia dongo Bahati, ambaye hivi karibuni alionekana kwenye video akiwa amevalia chupi ya kike. Mkali huyo wa ngoma ya Ngunga, amesema kwamba tabia kama hizo ni mfano mbaya kwa watoto na jamii kwa ujumla, akisisitiza kuwa wasanii wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa.

Kauli ya Willy Paul imetafsiriwa na mashabiki kama dongo kwa Bahati ambaye wiki hii amezua gumzo mtandaoni kutokana vitendo vyake vya kuvalia chupi ya kike na kunywa kinywa alichotumia kuosha miguu ya mke wake Diana Marua

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *