Entertainment

Msanii Alien Skin Anusurika Kifo Baada ya Kushambuliwa Jinja

Msanii Alien Skin Anusurika Kifo Baada ya Kushambuliwa Jinja

Msanii mwenye utata kutoka Uganda, Alien Skin, amenusurika kifo baada ya kushambuliwa na kundi la vijana wakorofi wakati wa ziara yake katika mji wa Jinja siku ya Alhamisi.

Mkali huyo wa ngoma ya Sitya Danger alikuwa amesafiri hadi mji huo kwa ajili ya kutumbuiza katika mkutano wa kisiasa wa chama cha NRM, lakini hali ilibadilika ghafla na vurugu kuzuka muda mfupi baada ya onyesho lake kumalizika.

Mashuhuda wanasema kuwa baadhi ya vijana waliokuwa kwenye umati waligeuka wenye fujo, jambo lililowalazimu polisi na waandaaji wa hafla hiyo kuingilia kati haraka kumwokoa msanii huyo. Alien Skin aliondolewa kwa dharura na kikosi chake cha usalama hadi sehemu salama.

Duru za kuaminika zinasema kuwa huenda tukio hilo lilichochewa na mivutano ya kisiasa, ikizingatiwa kuwa msanii huyo amewahi kutofautiana na wafuasi wa chama cha upinzani cha National Unity Platform (NUP) kinachoongozwa na Bobi Wine, ambaye ana ushawishi mkubwa katika eneo hilo.

Hii si mara ya kwanza kwa Alien Skin kukumbwa na vurugu katika eneo la mashariki mwa Uganda, mapema mwaka huu aliripotiwa kushambuliwa mjini Iganga baada ya onyesho jingine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *