 
									Msanii nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, ameondoa video na machapisho yote ya hivi karibuni kwenye mitandao yake ya kijamii yaliyomuonyesha akimuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan na chama tawala cha CCM.
Video hizo, ambazo zilikuwa zimeenea sana mtandaoni, zilionyesha Diamond akitumbuiza katika kampeni na ziara za kisiasa za Rais Samia na chama cha CCM, akionesha wazi uungwaji mkono wake kwa serikali na juhudi za rais huyo kutafuta muhula mwingine wa uongozi.
Hatua hii imekuja wakati ambapo Tanzania inakabiliwa na mzozo wa kisiasa na maandamano ya kumpinga Rais Samia, yaliyosambaa katika miji kadhaa ikiwemo Dar es Salaam, Arusha, na Mwanza. Maandamano hayo yamechochewa na madai ya kukandamizwa kwa viongozi wa upinzani na kukamatwa kwa wanaharakati.
Hadi sasa, Diamond hajatoa kauli rasmi kuhusu hatua yake, lakini wachambuzi wanasema anaweza kuwa anajitenga na lawama kutokana na mvutano wa kisiasa unaoendelea nchini humo.
 
								 
             
             
                             
                             
                             
                             
                             
                             
                            