Gossip

 Msanii Stevo Simple Boy Abarikiwa Mtoto wa Kiume na Mpenzi Wake Brenda

 Msanii Stevo Simple Boy Abarikiwa Mtoto wa Kiume na Mpenzi Wake Brenda

Msanii wa muziki kutoka nchini Kenya, Stevo Simple Boy na mpenzi wake Brenda, wamekaribisha mtoto wao wa kwanza, mvulana waliompa jina Dragon Junior.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Stevo ameshiriki picha akiwa pamoja na Brenda wakimkumbatia mtoto wao mchanga na kufahamisha mashabiki kuwa Dragon Junior amezaliwa salama. Pia ametoa shukrani kwa wafuasi wake kwa sapoti yao na kushiriki nambari yake ya mawasiliano kwa wale wanaotaka kumpa pongezi.

Taarifa hii imepokelewa kwa hisia mseto mitandaoni, ikizingatiwa kuwa imekuja siku chache baada ya baadhi ya wafuasi kuhoji uhalisia wa uhusiano wa Stevo na Brenda. Wengine walidai kuwa huenda Brenda hakuwa mke halisi wa msanii huyo, bali ni sehemu ya kiki za kutangaza kazi zake za muziki mtandaoni.

Hata hivyo, picha na ujumbe wa Stevo zimeonekana kuthibitisha kuwa wawili hao wamebarikiwa mtoto, hatua ambayo imezima uvumi uliokuwa ukienea kuhusu uhusiano wao. Mashabiki wamemiminika kwenye mitandao ya kijamii kumpongeza msanii huyo kwa hatua hiyo mpya katika maisha yake binafsi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *