Mtangazaji na mchekeshaji maarufu Oga Obinna ameahidi kumpeleka lunch date binti aliyesambaa mitandaoni baada ya kuonekana akimwaga machozi akieleza wazi mapenzi yake kwake kupitia video iliyosambazwa mitandaoni.
Binti huyo alionekana akieleza jinsi anavyompenda Obinna kwa moyo wake wote na kumwomba ampe nafasi ya kuwa naye, jambo lililozua maoni mseto mitandaoni.
Obinna kupitia ukurasa wake wa Instagram amejibu ujumbe huo akisema ameguswa na ujasiri wa binti huyo na kwamba atampatia nafasi ya kukutana naye ana kwa ana kwa ajili ya chakula cha jioni. Ameongeza kuwa anathamini mashabiki wake wote, na kwamba hatua hiyo ni njia ya kuonyesha shukrani kwa upendo na uungwaji mkono anaopokea kila siku.
Baadhi ya mashabiki wamepongeza hatua hiyo wakisema ni ishara ya utu na unyenyekevu wa Obinna, huku wengine wakidai huenda tukio hilo ni sehemu ya kiki ya mtandaoni.