Entertainment

Nasra Yusuf Akashifu Mastaa wa Bongo kwa Kushindwa Kukemea Maovu Tanzania

Nasra Yusuf Akashifu Mastaa wa Bongo kwa Kushindwa Kukemea Maovu Tanzania

Mchekeshaji wa Kenya, Nasra Yusuf, amewakosoa vikali wasanii nyota nchini Tanzania akiwemo Diamond Platnumz, Zuchu, Rayvanny, Harmonize, Alikiba, Mbosso, Juma Jux, Nandy na Jay Melody kwa kutozungumzia machafuko yanayoendelea nchini humo.

Kupitia ujumbe aliouchapisha mitandaoni, Nasra ameeleza kushangazwa na ukimya wa wasanii hao wakati ambapo mashabiki wao wanapitia mateso makubwa kutokana na vurugu na ukosefu wa usalama. Amesema kuwa vijana wengi nchini humo, hasa wanaowaona wasanii kama Diamond Platnumz kuwa mfano wa kuigwa, wanalia na kuteseka huku wengine wakipoteza maisha au kujeruhiwa kwa risasi, lakini wasanii hao hawajaonyesha mshikamano nao.

Nasra ameongeza kuwa ni jambo lisiloeleweka kuona wasanii hao wakiendelea kupromoti nyimbo zao katika kipindi ambacho mashabiki wao hawana amani wala utulivu wa kiakili wa kusikiliza muziki. Amesisitiza kuwa ni wajibu wa watu wenye majukwaa makubwa kutumia sauti zao kupaza sauti za wananchi wanaopitia mateso.

Aidha, amewakemea wasanii hao kwa kutochukua msimamo wakati vijana wao, mashabiki wao na watu wao wanawahitaji zaidi, akisema kuwa kimya chao kinaonyesha ukosefu wa utu na uwajibikaji. Ameonya kuwa hatua hiyo huenda ikaathiri uhusiano wao na mashabiki siku zijazo, kwani wananchi hawatasahau wale waliowaunga mkono wakati wa shida.

Nasra amehitimisha ujumbe wake Instagram kwa kuwataka wasanii wa Tanzania kuamka na kusimama na haki, akisisitiza kuwa sauti zao zina uzito mkubwa katika kuleta mabadiliko ya kijamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *