Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Marioo, ameungana na Watanzania katika kuomboleza vifo vya watu waliopoteza maisha kufuatia ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 29.
Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Marioo ameonyesha huzuni yake kwa matukio hayo na kutoa pole kwa familia, ndugu, na Watanzania wote walioguswa na vifo hivyo. Amesema kuwa taifa la Tanzania linapitia kipindi kigumu kinachohitaji umoja, subira, na maombi.
Msanii huyo ameongeza kuwa Mungu awape faraja wale waliopoteza wapendwa wao na kulitakia taifa la Tanzania amani na baraka.
Ujumbe wake umepokelewa kwa hisia tofauti, wengi wakimsifu kwa kuhubiri amani katika kipindi ambacho taifa linapitia mivutano ya kisiasa.