Entertainment

Mangi Kimambi Ataka Watanzania Kususia Shows za Wasanii Waliounga Mkono Rais Samia Hassan

Mangi Kimambi Ataka Watanzania Kususia Shows za Wasanii Waliounga Mkono Rais Samia Hassan

Mwanaharakati maarufu wa Tanzania Mangi Kimambi ametoa wito kwa Watanzania kususia maonyesho na matamasha ya wasanii wanaoonekana kuunga mkono serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Kupitia mitandao ya kijamii, Mangi amesema wasanii hao wamekuwa wakikaa kimya au hata kuwatetea viongozi licha ya wananchi kukabiliana na changamoto nyingi ikiwemo ukandamizaji wa haki za kiraia na vurugu zilizoshuhudiwa wakati wa maandamano.

Mangi ameongeza kuwa ni wakati sasa kwa wananchi kutumia nguvu yao ya kiuchumi kuwawajibisha wale wanaowapuuza.

Kauli hiyo imezua mjadala mkubwa mtandaoni, baadhi ya Watanzania wakikubaliana naye kwa kusema wasanii wanapaswa kusimama na wananchi, huku wengine wakipinga vikali wito huo wakisema sanaa haipaswi kuchanganywa na siasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *