WhatsApp hatimaye imezindua rasmi programu kamili kwa watumiaji wa Apple Watch, hatua inayowezesha sasa watumiaji kusoma na kujibu jumbe moja kwa moja kutoka kwenye saa zao.
Awali, Apple Watch ilikuwa inaruhusu arifa za jumbe pekee bila uwezo wa kujibu au kuona mazungumzo marefu. Hata hivyo, toleo jipya la programu hiyo limeleta huduma kamili ikiwemo kusoma jumbe ndefu, kurekodi na kutuma sauti, kutoa maoni kwa emoji, pamoja na kuona picha na stika kwa ubora zaidi.
Programu hiyo inapatikana kwa watumiaji wa Apple Watch Series 4 au matoleo mapya zaidi yanayoendesha mfumo wa watchOS 10 au juu yake.
Kwa hatua hii, watumiaji hawatalazimika tena kubeba simu kila wakati kwani sasa wanaweza kusoma, kujibu na kutoa hisia kwa jumbe za WhatsApp moja kwa moja kutoka kwenye Apple Watch yao.