Mrembo aliyekuwa ameamriwa na mahakama kumlipa mchekeshaji wa Kenya Oga Obinna fidia ya shilingi milioni 6 kwa kumdhalalisha, ameibuka akisema hana uwezo wa kulipa kiasi hicho kikubwa cha pesa.
Kupitia video inayosambaa mtandaoni, mrembo huyo alionekana akilia kwa uchungu, akieleza kuwa kwa sasa anapitia changamoto kubwa za kiuchumi na hana njia yoyote ya kupata fedha hizo.
Kesi hiyo ilitokana na madai kwamba mrembo huyo alitoa maneno ya kumdhalilisha Obinna kwenye mitandao ya kijamii, jambo lililomfanya mchekeshaji huyo kuchukua hatua za kisheria kulinda heshima yake.
Kwa sasa, mashabiki wa Obinna na watumiaji wa mitandao wametofautiana mitazamo, baadhi wakimtaka Obinna kumsamehe huku wengine wakisema sheria ichukue mkondo wake.