Gossip

Oga Obinna Atimiza Ahadi ya Kukutana na Binti Aliyemlilia Mtandaoni

Oga Obinna Atimiza Ahadi ya Kukutana na Binti Aliyemlilia Mtandaoni

Mtangazaji na mchekeshaji wa Kenya, Oga Obinna, hatimaye ameitikia wito wa mapenzi baada ya kutimiza ahadi yake ya kukutana na binti aliyemlia akimuomba penzi hadharani kupitia video iliyosambaa mitandaoni.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Obinna ameshiriki video ikimuonyesha akiwa kwenye chakula cha mchana na binti huyo, tukio ambalo limevutia hisia mseto kutoka kwa mashabiki wake.

Katika video hiyo, binti huyo anaonekana akiwa mwenye wasiwasi na mshangao mkubwa, akiwa haamini macho yake baada ya kukutana na mtu ambaye aliwahi kusema ni ndoto yake maishani. Obinna ameeleza kuwa wakati wa kwanza walipokutana, binti huyo alionekana mnyenyekevu na mwenye hofu, lakini baadaye hali ilirejea kawaida na wakaanza mazungumzo ya kirafiki.

Obinna amesema mtoko au date hiyo ilienda vizuri na walizungumza mambo mengi, ikiwemo namna atakavyoweza kumsaidia binti huyo ambaye alionyesha mapenzi ya dhati kwake kupitia video kwenye mtandao wa Tiktok.

Kabla ya mtoko huo, binti huyo alifanyiwa make-up kuboresha muonekano wake, huku akipata mavazi mapya yanayoendana na tukio hilo la kipekee kwenye moja ya spa ya kifahari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *