Gossip

Lydia Wanjiru Akanusha Tetesi za Kurudiana na Ex Wake Frank Dosoo

Lydia Wanjiru Akanusha Tetesi za Kurudiana na Ex Wake Frank Dosoo

Mrembo maarufu mtandaoni nchini Kenya, Lydia Wanjiru, amekanusha uvumi unaosambaa mtandaoni ukidai kuwa amerudiana na mpenzi wake wa zamani, Frank Dosoo.

Kupitia InstaStory yake, Lydia ameonekana kukanusha madai hayo kwa maneno makali, akisema kuwa anafurahia gossip kama wengine, lakini inapozidi mipaka inakuwa kero hasa pale ambapo watu wanatunga hadithi bila ushahidi. Amesisitiza kuwa katika ulimwengu wa sasa ambapo kesi za kisheria ni jambo la kawaida, ni muhimu watu kuzingatia ukweli na kuwa na ushahidi kabla ya kusambaza taarifa.

Mrembo huyo ameongeza kuwa madai ya kuonekana Kisumu akiwa na mtu fulani katika klabu moja ya usiku ni ya uongo, akibainisha kuwa hakuna hata picha au video inayoonyesha tukio hilo.

Kauli hiyo imezima tetesi zilizokuwa zikienea mitandaoni kwamba wawili hao wamefufua tena mahusiano yao, huku mashabiki wake wakimsifia kwa jinsi alivyochukua hatua ya kuweka wazi ukweli na kuepuka drama za mtandaoni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *