Mke wa msanii wa Arbantone VJ Patelo, anayejulikana kwa jina Dee, amethibitisha kuwa ni mjamzito kufuatia maswali ya mashabiki waliotaka kujua sababu ya kutokuonekana hadharani katika siku za hivi karibuni.
Kupitia ujumbe alioutoa kwenye mitandao ya kijamii, Dee amewaomba radhi mashabiki wake, hasa wale wa Lodwar, kwa kutojumuika nao katika matukio ya hivi karibuni na kueleza kuwa hali yake ya ujauzito imemlazimu kupumzika kwa muda.
Mwanamama huyo, amesema kuwa mashabiki wanapaswa kuelewa hali yake kwa sasa na akaahidi kwamba atashiriki kwenye matukio ya burudani mara atakapokuwa na nguvu za kutosha.
Kauli yake inakuja baada ya VJ Patelo kufanya club appearance wiki hii bila mke wake, hali iliyozua maswali kutoka kwa mashabiki waliotaka kufahamu sababu ya kutokuwepo kwake.