VJ Patelo Akerwa na Mashabiki Waliomtusi Mke Wake Kupitia TikTok Live
Msanii wa muziki wa Arbantone kutoka Kenya, VJ Patelo, ameonesha maumivu na hasira baada ya baadhi ya mashabiki kumtusi mke wake wakidai ana sura kombo wakati wa mazungumzo kupitia TikTok Live. Akijibu kwa ukali, VJ Patelo amewakemea waliotoa maneno hayo, akisema hawana haki ya kudharau mke wake wala kuingilia maisha yake binafsi. Ameeleza kuwa anampenda mke wake jinsi alivyo na hataruhusu mtu yeyote kumkashifu. VJ Patelo amesema iwapo kuna mtu anaona sura ya mke wake siyo nzuri, hilo halimhusu, akiwataka watu wajishughulishe na maisha yao badala ya kumdharau mtu ambaye yeye amechagua kumpenda. Katika mazungumzo hayo, VJ Patelo pia amejibu kwa hasira shinikizo kutoka kwa mashabiki waliomtaka arudi studio kuendelea na muziki. Amesema hana mpango wowote wa kurejea studio kwa sasa na akawaomba watu waache kufuatilia na kuingilia maisha yake binafsi.
Read More