Mchekeshaji wa Kenya kwa jina Dem wa Facebook ameonyesha kukerwa na tabia ya baadhi ya mastaa nchini humo wanaopenda kufanya “face reveal” za watoto wao kama njia ya kupata watazamaji au kujitafutia umaarufu mtandaoni.
Kupitia video iliyosambaa mitandaoni, Dem wa Facebook amesema kwamba mitindo hiyo haina maana kwa Wakenya, akisisitiza kuwa baadhi ya mastaa wamegeuza maisha yao binafsi kuwa maudhui ya mitandaoni bila kujali mipaka ya faragha.
Kulingana naye, tabia ya kuonyesha sura za watoto hadharani kwa minajili ya “likes” na “views” ni ishara ya kukosa busara na inaleta taswira mbaya kwa vijana na wazazi siku za usoni.
Hata hivyo Dem wa Facebook amewataka mastaa hao kuanza kushiriki maudhui yenye maana badala ya kuiga tamaduni za kigeni ambazo hazina umuhimu katika jamii.