Breaking!

Liverpool Yaangukia Pua Baada ya Kulazwa na Brighton 2-1
Instagram Yaleta Mabadiliko Mapya ya Reels kwa Urahisi Zaidi wa Watumiaji
Kai Havertz Aiokoa Arsenal Dakika za Lala Salama
Bahati Ataka Wakenya Waache Kumlaumu Kuhusu Matokeo ya DNA
April 26, 2026
  • Home
  • Briefs
  • Entertainment
  • Gossip
  • LifeStyle
  • Tech
  • Sports

Tag: Dem wa Facebook

 Dem wa Facebook Akataa Kuweka Wazi Baba wa Mtoto
Robert Elim February 2, 2026
Comments (0)

Dem wa Facebook Akataa Kuweka Wazi Baba wa Mtoto

Content creator kutoka Kenya, Dem wa Facebook amekataa kuweka wazi jina la mwanaume aliyempa ujauzito baada ya mashabiki kuendelea kumuuliza ni nani baba wa mtoto anayemtarajia. Kupitia mitandao ya kijamii, Dem wa Facebook amesema ujauzito wake ni jambo la binafsi na hahitaji kuthibitisha au kueleza chochote kwa umma licha ya umaarufu wake mitandaoni. Mrembo huyo, ameeleza kuwa anachochagua kushiriki ni maisha yake binafsi kwa kiwango anachokiona kinafaa, na si kila kitu lazima kiwekwe hadharani. Kauli yake imekuja mara baada ya kuwataarifu mashabiki zake kuwa anatarajiwa kupata mtoto hivi karibuni, taarifa iliyozua mjadala mkubwa mitandaoni. Hata hivyo, licha ya pongezi kutoka kwa baadhi ya mashabiki, wapo watu waliotilia shaka madai hayo na kudai huenda ni njia ya kuvutia hisia za umma.

Read More
 Dem Wa Facebook Atangaza Nia ya Kugombea Uwakilishi wa Wanawake 2027
Robert Elim January 28, 2026
Comments (0)

Dem Wa Facebook Atangaza Nia ya Kugombea Uwakilishi wa Wanawake 2027

Mtayarishaji wa maudhui mtandaoni, Dem Wa Facebook, ametangaza rasmi nia yake ya kugombea kiti cha Mwakilishi wa Wanawake katika Uchaguzi Mkuu nchini Kenya wa mwaka 2027. Kupitia ukurasa zake za mitandao ya kijamii, Dem Wa Facebook ameposti bango la kampeni lililoambatana na ujumbe ulioibua mjadala mkubwa mtandaoni, akiwahoji wananchi iwapo mwaka 2027 ni wakati mwafaka kwake kuwania nafasi hiyo au kama anapaswa kusubiri hadi 2032 baada ya kura kuchukuliwa. Katika tangazo hilo, Dem Wa Facebook ameweka wazi vipaumbele vya manifesto yake ambavyo vinajikita katika uwazi na uwajibikaji, kuinua uchumi wa wanawake, kuwawezesha vijana kiuchumi na kijamii, pamoja na kuhakikisha kunakuwepo uwakilishi wa haki na sauti halisi katika uongozi. Hatua hii inamuweka Dem Wa Facebook miongoni mwa wanawake wanaojitokeza kuwania nyadhifa za uongozi kuelekea uchaguzi wa 2027, hali inayodhihirisha mabadiliko ya kisiasa yanayoendelea nchini Kenya, hususan kuibuka kwa viongozi wapya wanaotumia majukwaa ya mitandao ya kijamii kufikisha ajenda zao kwa umma.

Read More
 Dem wa Facebook Akemea Mastaa  wa Kenya kwa Kuonyesha Nyuso za Watoto Mitandaoni
Robert Elim November 10, 2025
Comments (0)

Dem wa Facebook Akemea Mastaa  wa Kenya kwa Kuonyesha Nyuso za Watoto Mitandaoni

Mchekeshaji wa Kenya kwa jina Dem wa Facebook ameonyesha kukerwa na tabia ya baadhi ya mastaa nchini humo wanaopenda kufanya “face reveal” za watoto wao kama njia ya kupata watazamaji au kujitafutia umaarufu mtandaoni. Kupitia video iliyosambaa mitandaoni, Dem wa Facebook amesema kwamba mitindo hiyo haina maana kwa Wakenya, akisisitiza kuwa baadhi ya mastaa wamegeuza maisha yao binafsi kuwa maudhui ya mitandaoni bila kujali mipaka ya faragha. Kulingana naye, tabia ya kuonyesha sura za watoto hadharani kwa minajili ya “likes” na “views” ni ishara ya kukosa busara na inaleta taswira mbaya kwa vijana na wazazi siku za usoni. Hata hivyo Dem wa Facebook amewataka mastaa hao kuanza kushiriki maudhui yenye maana badala ya kuiga tamaduni za kigeni ambazo hazina umuhimu katika jamii.

Read More
 Dem wa Facebook’ Asema Hajui Sababu ya Kipindi Chake na Oga Obinna Kusitishwa
Robert Elim October 7, 2025
Comments (0)

Dem wa Facebook’ Asema Hajui Sababu ya Kipindi Chake na Oga Obinna Kusitishwa

Mchekeshaji maarufu mtandaoni Dem wa Facebook ameeleza kuwa hajui sababu kamili ya kusitishwa kwa kipindi chake cha kila wiki alichokuwa akiendesha na Oga Obinna, akisema uamuzi huo ulitokea ghafla bila maelezo yoyote rasmi. Kwa mujibu wa Dem wa Facebook, wao walikuwa wakirekodi kipindi hicho kila Jumatatu, lakini wiki iliyofuata hakupokea ujumbe wowote kutoka kwa PA wa Obinna, hali iliyomfanya kuamini kwamba huenda kulikuwa na mabadiliko ya mipango au mtangazaji huyo aliamua kushika wasanii wengine mkono. Akipiga stori na Podcast ya Mwakideu Live, amesema kuwa hakuwa amepokea taarifa yoyote ya kufutwa kwa show hiyo, na alitarajia kuwa wangeendelea kurekodi kama kawaida. Kipindi hicho, ambacho kilikuwa kikipata umaarufu mkubwa kwa ucheshi na mijadala ya kijamii, kiliwavutia watazamaji wengi mitandaoni kutokana na utani na urafiki wa kipekee kati ya Dem wa Facebook na Oga Obinna.

Read More

About Urban Spice

UrbanSpice.ke is Kenya's flavor-packed digital hub, delivering the hottest Entertainment, Sports, and Tech stories with a bold twist.

🔥 Spice Up Your Daily Buzz- One headline at a time.

Quick Links

  • Home
  • Briefs
  • Entertainment
  • Gossip
  • Lifestyle
  • Tech
  • Sports
  • Contact Us ▼
    • 📧 info@urbanspice.ke
    • 📧 urbanspice254@gmail.com
    • 📞 0750 396 709
    • 💬 Chat on WhatsApp

Follow Us

Stay in the loop with the latest buzz.

Contact Us

Email 1:info@urbanspice.ke

Email 2:urbanspice254@gmail.com

Phone: 0750 396 709

WhatsApp: Chat on WhatsApp

© 2025 UrbanSpice.ke — All rights reserved.