Entertainment

Bahati Ajigamba Kuwa Msanii Pekee Kenya Mwenye Nyimbo Tatu Zinazotrend YouTube

Bahati Ajigamba Kuwa Msanii Pekee Kenya Mwenye Nyimbo Tatu Zinazotrend YouTube

Msanii asiyeishiwa na matukio kila leo, Bahati, ameibuka tena mtandaoni akijigamba kuwa ndiye msanii pekee nchini Kenya mwenye nyimbo tatu zinazotamba kwenye orodha ya video kumi bora zaidi kwenye mtandao wa YouTube.

Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Bahati ameeleza kuwa anajivunia mafanikio hayo makubwa katika muziki wake, akisema ni heshima kubwa kwake kuona nyimbo tatu zake zikiwa zinatrend kwa wakati mmoja.

Kauli yake imekuja muda mfupi baada ya nyimbo zake “First Love,” “Umenipendelea,” na “Bye Bye Baba” kuingia katika chati za ngoma zinazovuma nchini Kenya kwenye mtandao wa YouTube.

Bahati ameendelea kuonyesha kuwa bado ana ushawishi mkubwa katika muziki wa kizazi kipya, huku mashabiki wake wakimpongeza kwa juhudi na uthabiti anaouonyesha licha ya changamoto na mijadala inayomzunguka mara kwa mara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *