Msanii wa muziki wa Bongofleva, Best Naso, amewaomba mashabiki wake kumsaidia kutafsiri ndoto aliyoita ya kutisha na ya ajabu baada ya kuiota akiwa kwenye mji usio wa kawaida.
Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Best Naso ameeleza kuwa katika ndoto hiyo alijikuta akiwa katika mji wenye uwanja mkubwa, ambapo masheikh walikuwa wakichomwa moto huku hakuna mtu wa kawaida aliyekuwepo eneo hilo.
Kulingana na maelezo yake, jambo lililomshangaza zaidi ni kuwa baadhi ya masheikh aliowaona akiwashwa moto ni wale anaowafahamu katika maisha halisi.
Msanii huyo amesema ndoto hiyo imemwacha na maswali mengi, akiwataka mashabiki wake wenye uelewa kuhusu tafsiri za ndoto kumsaidia kuelewa maana yake.