Entertainment

Mke wa Guardian Angel Afunguka Kuhusu Matusi Mtandaoni

Mke wa Guardian Angel Afunguka Kuhusu Matusi Mtandaoni

Mke wa mwimbaji wa Injili Guardian Angel, anayefahamika kama Esther Musila, ameapa kupambana vikali na wakosoaji wake mtandaoni hadi mwisho wa dunia.

Kupitia ukurasa wake wa TikTok, Musila amesisitiza kuwa hatakubali kunyamaza huku akivunjiwa heshima mtandaoni bila kujibu.

Mwanamama huyo ameonyesha hasira yake kwa watu wanaojiona wana uwezo wa kudhibiti maisha ya watu wengine, akisema wazi kwamba atajibu matusi kwa matusi inapobidi.

Kauli hiyo imekuja kufuatia mijadala iliyoanzishwa na madai ya msanii, Shiru wa GP ambaye hivi karibuni alidai kuwa marehemu Betty Bayo aliogopa sana hali yake ya kiafya kujulikana kwa umma kutokana na hofu ya kuhukumiwa. Shiru wa GP alidai kuwa hofu ya Betty Bayo ilitokana na jinsi alivyokuwa amedhalilishwa na kuhukumiwa mtandaoni miaka kadhaa iliyopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *