Entertainment

Pritty Vishy Akanusha Kutumia Uhusiano na Stevo Simple Boy Kutafuta Umaarufu

Pritty Vishy Akanusha Kutumia Uhusiano na Stevo Simple Boy Kutafuta Umaarufu

Mwanamitindo na mshawishi wa mitandaoni, Pritty Vishy, amejibu madai ya msanii Stevo Simple Boy kwamba alitumia uhusiano wao wa kimapenzi kama njia ya kujitafutia umaarufu.

Akipiga stori na Podcast ya Mylee Staicey, Pritty Vishy amesema madai hayo hayana msingi wowote, akisema Stevo ndiye aliyewahi kukataa dili la mamilioni ya fedha kutoka kwa kampuni mmoja iliyotaka kumdhamini.

Kwa mujibu wa Vishy, kampuni hiyo ilikuwa tayari kumlipa Stevo kiasi kikubwa cha fedha, lakini msanii huyo alikataa ofa hiyo baada ya kusikia kuwa walitaka wafanye naye pamoja.

Amesema haelewi ni kwa nini Stevo sasa anadai alitumia jina lake kupata umaarufu, ilhali kuna ushahidi kuwa kipindi cha uhusiano wao, alijitolea kumsaidia na hata kuhusika kwenye baadhi ya maamuzi muhimu ya kazi yake.

Pritty Vishy ameongeza kuwa hajawahi kutafuta umaarufu kupitia mgogoro na anamtakia Stevo mema, lakini hakutaka kimya chake kitafsiriwe vibaya kuhusu maisha yao ya zamani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *