Meta imetangaza kuwa WhatsApp itaanza kuruhusu watumiaji wa barani Ulaya kutuma na kupokea jumbe kutoka apps nyingine kama BirdyChat na Haiket.
Watumiaji wataweza kutuma text, picha, sauti, video na files kwa watumiaji wa apps nyingine. Hii itasaidia watu kutumiaji wa apps nyingine kuwa na uwezo wa kuchat na watumiaji wa WhatsApp bila kulazimika kuwa na WhatsApp. Pia itasaidia wale ambao hawapendi kutumia app ya WhatsApp.
Mabadiliko haya yatakuwa na limit mfano itakuwa ni kwa watumiaji wa apps za simu tu na sio app za kompyuta au website. Mfumo wa encryption utabaki kuwa salama na mtu anaweza kuchagua chats za watumiaji wa apps nyingine zijichanganye na chats za WhatsApp au kutengeneza folder za kutenganisha chats.
Kwa kawaida, kiteknolojia jambo hili linawezekana na pia ni rahisi kuunganisha lakini kampuni nyingi za mitandao hazipendi kuweka feature hii kwa kuhofia kupoteza soko lake.