Mwanamuziki Bien kutoka kundi la Sauti Sol ameibua mjadala mtandaoni baada ya kueleza mtazamo wake binafsi kuhusu namna angetaka kuzikwa endapo siku yake ya kuaga dunia itawadia.
Katika maelezo yake, Bien amesisitiza kuwa hataki kabisa kufukiwa kaburini, akiamini kuwa kaburi ni upotevu wa ardhi na sio njia anayopendelea.
Mkali huyo wa All My Enemies Are Suffering, amesema kuwa iwapo ataondoka duniani, angetaka mwili wake uchomwe na majivu yake yatupwe baharini au yahifadhiwe kwenye kifaa kama hourglass ili familia iweze kutumia kwa shughuli za kawaida au michezo.
Hata hivyo, Bien amesisitiza kuwa huu ni msimamo wake binafsi na angependa uheshimiwe kama ilivyo, jambo linaloibua mjadala mpana kuhusu namna watu wanavyotaka kukumbukwa baada ya maisha yao duniani.