Entertainment

Luciano Ataka Rais William Ruto Kuhalalisha Bangi Kenya

Luciano Ataka Rais William Ruto Kuhalalisha Bangi Kenya

Msanii nyota wa reggae kutoka Jamaica, Luciano, ameibua mjadala mzito mtandaoni baada ya kumtaka Rais William Ruto kuzingatia hatua ya kuifanya Kenya kuwa miongoni mwa nchi za kwanza barani Afrika kuhalalisha bangi.

Akizungumza na Radio Citizen, Luciano amesifu ushawishi mkubwa wa kitamaduni wa Kenya barani Afrika na duniani, akisema kuwa uhalalishaji wa bangi unaweza kufungua milango mipya ya kiuchumi na kitabibu.

Kwa mujibu wa msanii huyo, nchi zilizoidhinisha matumizi ya bangi kwa udhibiti maalum zimefaidika kupitia ongezeko la mapato ya serikali, kupanuka kwa sekta ya kilimo, na maendeleo katika tafiti za tiba mbadala.

Hata hivyo, msanii huyo ambaye kwa sasa yuko nchini Kenya kwa ziara yake ya muziki, amesisitiza kuwa uamuzi kuhalalisha bangi unaweza kuibadilisha Kenya kiuchumi na kuiweka katika ramani ya kimataifa kama taifa linaloongoza katika mageuzi ya kisera.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *