Influencer na content creator kutoka Kenya Pritty Vishy amejibu vikali ukosoaji unaoendelea mitandaoni dhidi ya mastaa wanaochagua kufanyiwa upasuaji wa urembo, akiwataka Wakenya kuacha kuwahukumu bila kuelewa ukweli wa mambo.

Katika ujumbe wake aliyouweka mtandaoni, Pritty Vishy ameweka wazi kuwa maamuzi ya mtu kuhusu mwili wake ni ya kibinafsi na hayapaswi kugeuzwa chanzo cha mashambulizi ya mtandaoni.

Ameeleza kuwa wengi wanaotoa maoni mazito mara nyingi hawana taarifa sahihi kuhusu sababu zinazowasukuma watu kuchagua njia hizo, ikiwemo afya ya kiakili, kujiamini, na malengo ya kibinafsi.

Mrembo huyo amesema pia ni muhimu kwa umma kufanya utafiti wa kina na kuelewa kilicho nyuma ya maamuzi ya mtu kabla ya kutoa hukumu za haraka au kuashiria kwamba influencers wanafuata mitindo bila kufikiria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *