Entertainment

Msanii Mkongwe wa Reggae Jimmy Cliff Afariki Dunia

Msanii Mkongwe wa Reggae Jimmy Cliff Afariki Dunia

Nguli wa muziki wa reggae duniani, Jimmy Cliff, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 81. Familia yake ilithibitisha taarifa hizo jana, ikieleza kuwa alifariki baada ya kupata mshituko (seizure) uliotanguliwa na pneumonia.

Jimmy Cliff, ambaye amekuwa mmoja wa wasanii tajika katika historia ya reggae, alijizolea umaarufu kupitia vibao kama “Many Rivers to Cross”, “Wonderful World, Beautiful People”, na nyimbo nyingine ambazo zimevuka vizazi na mipaka ya mataifa.

Msanii huyo mzaliwa wa Jamaica mwaka 1944 alikuwa sio tu mwimbaji, bali pia mwandishi wa nyimbo, muigizaji na balozi wa utamaduni wa reggae kote ulimwenguni. Kazi zake zimekuwa msukumo kwa wasanii wengi wa sasa na mashabiki wa muziki wa roots reggae, ska, na rocksteady.

Mashabiki, wanamuziki wenzake na viongozi kutoka maeneo mbalimbali ya dunia wameendelea kumiminika mitandaoni kutoa salamu za rambirambi na kusherehekea maisha ya gwiji huyo.

Kifo cha Jimmy Cliff ni pigo kubwa kwa ulimwengu wa muziki, lakini urithi wake utaendelea kuishi kupitia nyimbo na ujumbe wake uliogusa mioyo ya mamilioni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *