Sociliate mwenye asili ya Uganda, Zari Hassan, ameibua mjadala mtandaoni baada ya kusema kuwa mume wake Shakib huvutia idadi kubwa ya wanawake.
Kulingana na Zari, kivutio cha Shakib kwa wanawake hakitokani na mvuto wake binafsi, bali kinachochewa zaidi na hadhi yake kama mume wa mtu maarufu.
Mwanamama huyo, ambaye ni mmoja wa socialite wenye ushawishi mkubwa barani Afrika, ameongeza kuwa mara nyingi wanawake humfuata Shakib kwa udadisi, wakitaka kufahamu ni nini hasa alichokiona kwake hadi wakafunga ndoa.
Kauli hiyo imezua maoni mseto kutoka kwa mashabiki, baadhi wakisema Zari amekuwa akizungumza kwa ujasiri na kwa mtindo wake wa kawaida wa kuchokoza mjadala, huku wengine wakiona maneno yake kama ishara ya kujiamini na kumthamini mume wake.
Shakib na Zari wamekuwa katika uhusiano wa hadharani kwa muda, na mara kadhaa wamekuwa wakionekana wakioneshana mapenzi mtandaoni na kwenye vyombo vya habari. Hata hivyo, uhusiano wao umekuwa ukivutia mjadala kutokana na tofauti zao za umri na maisha yao ya hadhara.