Tech news

YouTube Yajaribu Kurudisha Sehemu ya Meseji Moja kwa Moja

YouTube Yajaribu Kurudisha Sehemu ya Meseji Moja kwa Moja

YouTube imeanza kujaribu kurudisha huduma ya ujumbe wa moja kwa moja, inayojulikana kama DM, kwenye app yake ya simu.

Sehemu hii iliondolewa mwaka 2019, lakini kampuni hiyo imesema watumiaji wengi walikuwa wanaiomba irudishwe. Sasa YouTube imeanza kufanya majaribio kwa baadhi ya watumiaji wenye umri wa miaka 18 na kuendelea.

Kwa mfumo huu mpya, watumiaji wataweza kutuma meseji, links, video fupi, live videos na video ndefu, sawa na jinsi inavyofanya WhatsApp au Instagram DM. Mtu ambaye haujachat naye anaweza kukubali au kukataa ujumbe wako, na kuna kikomo cha kutuma meseji kwa akaunti ambazo hazijawahi kuzungumza na wewe.

Facebook, TikTok, Instagram, X na platform nyingine nyingi tayari zina huduma ya DM, na inaonekana YouTube imeona ni muhimu kurudisha huduma hii kufuata mahitaji ya watumiaji

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *