Entertainment

Nadia Mukami Aikosoa Orodha ya WCB Kuhusu Wasanii wa Kike Wanaotazamwa Zaidi YouTube

Nadia Mukami Aikosoa Orodha ya WCB Kuhusu Wasanii wa Kike Wanaotazamwa Zaidi YouTube

Mwanamuziki kutoka Kenya Nadia Mukami ameikosoa lebo ya WCB Wasafi kwa kumwacha nje ya orodha ya wasanii wa kike kutoka Afrika Mashariki wenye watazamaji wengi zaidi kwenye YouTube.

Nadia, ambaye kwa sasa ana zaidi ya watazamaji milioni 118 kwenye chaneli yake, ameeleza kuwa orodha hiyo ni batili na haina uhalali kwa sababu haijazingatia takwimu zake ambazo zinamweka miongoni mwa wasanii wanaoongoza katika ukanda huu.

Katika ujumbe wake, ameonesha kutoridhishwa na kile alichokitaja kama kupuuzwa kwa mchango wake katika muziki wa Afrika Mashariki, akisisitiza kuwa juhudi zake na ukuaji wa chaneli yake haviwezi kupuuzwa katika tathmini kama hiyo.

Aidha, Nadia ametoa wito kwa mashabiki wake kuendelea kuiunga mkono safari yake ya kutimiza lengo la kufikisha wafuatiliaji milioni moja kwenye chaneli yake ya Youtube.

Tukio hili limezua mjadala mpana mtandaoni, mashabiki wengi wakitafsiri hatua ya Nadia kama mwito kwa wadau wa muziki kutambua takwimu halisi na mchango wa wasanii wa kike wanaotoka nje ya lebo kubwa za muziki katika kanda ya Afrika Mashariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *