Entertainment

Bensoul na Vic West Watangaza Ujio wa EP Mpya

Bensoul na Vic West Watangaza Ujio wa EP Mpya

Wanasani wa muziki wa kizazi kipya nchini Kenya, Bensoul na Vic West, wametangaza rasmi ujio wa EP yao mpya iitwayo “All Hands on Dec”

Kupitia mitandao yao ya kijamii wawili hao, wamethibitisha kuwa mradi huu una jumla ya nyimbo saba za moto na itaingia sokoni Disemba 5 mwaka huu 2025.

Kwa mujibu wa artwork walioshiriki mtandaoni, EP hiyo itajumuisha ushirikiano wa wasanii mbali mbali kama Tipsy Gee, Malosh, Ssaru, Mordecai Dex, Ndovu Kuu, Harry Craze, na Fathermoh, ambao wataleta mitindo na sauti tofauti yenye ubunifu.

EP ya “All Hands on Dec” inatarajiwa kupatikana kwenye majukwaa yote makubwa ya muziki mtandaoni, ikiwemo Spotify, Apple Music, na YouTube Music, na tayari imeanza kuzua shauku kubwa kwa mashabiki wa muziki wa Kenya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *