Tech news

ChatGPT Kuanza Kuonyesha Matangazo kwa Watumiaji wa Bure

ChatGPT Kuanza Kuonyesha Matangazo kwa Watumiaji wa Bure

Kampuni ya OpenAI inajipanga kuanza kuweka matangazo kwa watumiaji wa bure wa ChatGPT, ikiwa ni sehemu ya mpango mpya wa kuongeza mapato.

Taarifa zinaonyesha kuwa mfumo mpya wa apps za ChatGPT umeanza kuonyesha misimbo ya aina mbalimbali za matangazo, ikiwemo search ads, ad carousel na hata API maalum ya kuendesha matangazo hayo. Mpango huo unatarajiwa kuenea kwenye majukwaa ya iOS, Mac pamoja na toleo la tovuti.

Hatua hii inaelezwa kuwa njia ya kuimarisha mapato, hasa kwa kuwa huduma za Plus zinazotozwa dola 20 kwa mwezi na Pro dola 200 kwa mwezi, hazina matangazo na zinategemea ada za wanachama. Aidha, kuna dalili za kupandishwa bei kwa baadhi ya huduma za kulipia.

Kwa sasa, matangazo yanaripotiwa kuonekana zaidi katika kitengo cha search, na hasa pale watumiaji wanapouliza maswali yahusuyo bidhaa za kununua.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *